Vijana wasiokuwa na elimu kujadiliana na Ahl-ul-Bid´ah


Swali: Kuna kijana ambaye wakati mwingine anahitajia kujadiliana na Ahl-ul-Bid´ah katika mji wake. Je, inajuzu kwake kufanya hivo?

Jibu: Kijana ambaye hana elimu anataka kujadiliana na Ahl-ul-Bid´ah matokeo yake waje kumshinda halafu aje kuufedhehesha Uislamu na waislamu! Kwa ajili hii ndio maana Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na wengineo wamesema:

“Kwa kuwa si haki kwa mjinga kujadiliana na Ahl-ul-Bid´ah akaja kuuangusha Uislamu.”

Anajitokeza mtu na kujiita Salafiy ambapo anajadiliana na mzushi ilihali hana elimu na upande mwingine hasimu wake ana shubuha na dalili anazowatatiza kwazo watu na isitoshe anafuata zile dalili sizizokuwa wazi. Hatimaye hasimu wake anamshinda na anakuwa ameiangusha Sunnah na haki. Mtu huyu asisababishe kuudhoofisha Uislamu.

Tukisema uache kujadiliana haina maana kwamba uache kufanya Da´wah, kufanya bayana, kuandika n.k. Hapana, sivyo ninavyomaanisha. Mijadala ina njia zake maalum.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/questions.php?cat=26&id=611
  • Imechapishwa: 16/03/2018