Vijana wanasikiliza mihadhara ya Hizbiyyuun inayozilainisha nyonyo

Swali: Ni ipi hukumu ya kusikiliza mihadhara inayoathiri ya watoa mawaidha ambao ni Hizbiyyuun au watu ambao hawatambuliki pamoja na kuzingatia kwamba vijana wengi hawana elimu inayotosha kuweza kupambanua kati ya yaliyo ya sawa na ya makosa?

Jibu: Yaliyotoka kwa Salaf wa kale na waliokuja nyuma yanatosheleza. Ni lazima kushikamana nayo. Kwa sababu hatuna haja ya watu wazushi na ambao wanaeneza mawaidha na visa vinavyovutia. Katika elimu ya Salaf kuna ambayo yanatosheleza. Huo ndio wajibu wetu sisi na nyinyi.

Wanafunzi, waarabu na wasiokuwa waarabu, wanatakiwa kunasihiwa kushikamana na elimu ya Salaf, mawaidha ya Salaf na vitabu vya Salaf. Ndani yake kuna kheri kamilifu, kama mlivyopitia na mkasikia dalili.

Allaah amewasifu Salaf na wafuasi wao sifa lukuki na hakufanya hivo isipokuwa ni kwa sababu wako juu ya uongofu na haki ya wazi. Haya ndio niliyotaka kukwambieni.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://sahab.net/forums/showthread.php?t=331010
  • Imechapishwa: 27/11/2020