Swali: Kumejitokeza kundi la vijana wanamfanyia Tabdiy´ Abu Haniyfah, wanawakufurisha Ashaa´irah na wamekithirisha kumraddi adh-Dhahabiy na al-Khattwaabiy…

Jibu: Hawa ima ni wajinga au wapotevu. Abu Haniyfah ni katika maimamu wa Ahl-us-Sunnah. Ni katika maimamu wa mwanzo kabisa wa Ahl-us-Sunnah baada ya Maswahabah na Taabi´uun. Yeye ndiye wa mwanzo kabisa katika wale maimamu wane. Amechukua elimu kutoka kwa Taabi´uun. Imesemekana vilevile ya kwamba amechukua elimu kutoka kwa Maswahabah. Ima ni Taabi´iy au ni katika wale waliokuja baada ya Taabi´uun. Ana kutangulia katika Uislamu, uelewa, ´ibaadah na uchaji. Haijuzu. Huyu ni katika maimamu wa waislamu. Ukimtukana mmoja wa maimamu wa waislamu umewatukana waislamu. Haijuzu kufanya hivi. Hatusemi kuwa hana makosa, makosa yanatokea, lakini ´Aqiydah yake na mfumo wake ni salama. Kuhusu kukosea inapokuja katika baadhi ya mambo ya Ijtihaad, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anapohukumu hakimu na akapatia, basi ana thawabu mara mbili. Na anapohukumu na akakosea, basi ana thawabu mara moja.”

Unapomtukana mmoja wa maimamu wa waislamu, sawa awe ni Abu Haniyfah au mwengine, umeutukana Uislamu. Kitendo cha wanachuoni wengine kuwa na baadhi ya makosa, haina maana kwamba ipelekee wazingatiwe kuwa ni wapotevu au watu wa Bid´ah. Wamekosea na Allaah awasamehe, lakini elimu yao iliyobobea, uelewa wao, utambuzi wao wa Hadiyth ni mkubwa kuliko makosa wanayoweza kuwa nayo. Mtu asitafute na kupekua aibu za watu na kasoro za wanachuoni. Hivi ndivyo wanavyofanya wapindaji na wapotevu wanaowakimbiza watu kutokamana na Uislamu na wanachuoni. Endapo utamchunguza huyu anayezungumza namna hii utaona kuwa ana makapu ya makosa na kasoro. Lakini hayaoni makosa yake mwenyewe. Utamuona kuwa ni mjinga asiyejielewa. Yeye mwenyewe kitu katika elimu. Pamoja na hivyo anawakosoa wanachuoni na maimamu. Hii ni njia ya makosa. Haijuzu kuongea kwa namna hii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=hulsbk4cM9o
  • Imechapishwa: 29/01/2017