Vidonge vinavyozuia kushika mimba katika Ramadhaan


Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kutumia vidonge vinavyositisha hedhi au kuzuia kushika mimba katika Ramadhaan?

Jibu: Hakuna neno kwa sharti si vyenye kumdhuru mwanamke. Hakuna neno kwa mwanamke kutumia vidonge vinavyozuia kushika mimba kwa muda au vinavozuia hedhi ili aweze kufunga au kutokana na sababu nyingine, kama alivyothibitisha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na wengineo. Hata hivyo itakuwa haijuzu ikiwa kule kuvitumia kunamdhuru mwanamke – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin Humayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Ibn Humayd, uk. 175
  • Imechapishwa: 05/05/2021