Vidonge dhidi ya hedhi kwa ajili ya kufanya ´ibaadah

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwanamke kutumia dawa za kuzuia ada yake ya mwezi ili aweze kufunga Ramadhaan yote?

Jibu: Hakuna neno. Akiwa hana mashaka nazo na hazimdhuru, hakuna neno. Lakini hata hivyo bora ni kuacha kuzitumia[1].

Swali: Je, anaweza kuzitumia kwa ajili ya kufanya ´umrah au hajj?

Jibu: Ni sawa endapo atazitumia kabla ya kuanza kutokwa na ada yake ya mwezi. Lakini kama tayari ameshatokwa na ada yake ya mwezi vidonge hivi havisaidii kitu.

[1] https://firqatunnajia.com/ibn-uthaymiyn-anakataza-kutumia-dawa-za-kuzuia-hedhi-kutokana-na-madhara-yake/ 

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (18) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtfq-15011435-01.mp3
  • Imechapishwa: 23/11/2019