Swali: Je, kuna sharti kwa mwanamme kuvaa pete ya fedha au kuna hali maalum?

Jibu: Hapana. Aivae kwenye kidole kidogo au kidole cha pete kwenye mkono wa kulia au kwenye mkono wa kushoto. Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivaa pete kwenye kidole cha pete. Kwa hiyo aivae kwenye kidole kidogo au kidole cha pete. Kuhusu kidole cha katikati na kidole cha kuashiria asivae. Imeruhusiwa kuvaa pete ya fedha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 21/11/2021