Vidogonge vya kuzuia mimba vinasababisha mvurugo wa ada ya mwezi

Swali: Mwanamke alitumia tembe za kuzuia mimba ambapo hedhi yake ikawa inakuja ikikatikatika. Kuna wakati inamjia mara moja kwa siku. Je, aswali wakati amekauka?

Jibu: Kama damu inamjia wakati mfupi, haina hukumu; atatakiwa kuswali. Damu hii haina hukumu. Lakini kama inamjia siku nzima au mchana na usiku wake, inazingatiwa ni hedhi. Hivyo itambidi aache swalah kipindi inamjia. Inapokatika atajisafisha na kuswali.

Mimi nawanasihi wanawake wasijiadhibu kwa kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, tembe na vyenginevyo. Kwa sababu vitu kama hivi vinamdhuru na vinamweka katika mashaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (21) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2020