Swali: Wafanyikazi wa kituruki na wa kisyria ni Nusayriyyah lakini kwenye pasipoti na vitambulisho vyao imeandikwa kwamba ni waislamu. Wafanya kazi sehemu za machinjio, migahawa na sehemu nyenginezo. Je, inafaa kula katika vichinjwa vyao?

Jibu: Inatakiwa kutazama Bid´ah za Nusayriyyah na Ahl-ul-Bid´ah wengineo. Ikiwa Bid´ah zao ni za ukafiri, basi haijuzu kula katika vichinjwa vyao. Kwa sababu haijuzu kula katika vichinjwa vya makafiri isipokuwa tu vichinjwa vya mayahudi na manaswara.

Ama ikiwa Bid´ah zao sio za ukafiri, basi hapana neno kwetu kula vichinjwa vyao. Lakini hata kama Bid´ah zao sio za ukafiri bora ni kula nyama za wengine.

Swali: Nini anachosema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah juu ya Nusayriyyah?

Jibu: Udhahiri ni kwamba Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) anawakufurisha. Wakiwa ni makafiri ni kama nilivyosema kwamba haijuzu kula vichinjwa vyao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (5 B)
  • Imechapishwa: 14/07/2021