Vibao vilivyoandikwa (الله) na (محمد)

Jengine ni kwamba vibao vilivyoandikwa “Allaah” na pembezoni mwake “Muhammad” ni aina fulani ya ushirikiano na kumlinganisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), jambo ambalo halifai. Kuna mtu alisema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

ما شاء الله وشئت

“Akitaka Allaah na wewe.”

 Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Je, umenifanya kuwa mshirika wa Allaah? Sema: “Akitaka Allaah pekee.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (01) http://binothaimeen.net/content/6625
  • Imechapishwa: 01/02/2019