Vibanio vya nywele na nywele kufanya nundu kwenye mtandio


Swali: Kuna msichana wa masomoni ambaye nywele zake ni ndefu na akizikusanya na kuweka kibanio zinafanya ´Abaa´ah kuinuka kwa juu mbele ya wanaume. Je, kitendo hichi kinafaa pamoja na kuzingatia kwamba sijafanya hivo ili wanaume wanitazame?

Jibu: Akifanya hivo ili wanaume wamtazame hapana shaka kwamba kitendo hicho ni kujishaua kwa kuonyesha mapambo. Kitendo hicho hakijuzu. Kinapelekea katika fitina. Ama ikiwa ni chini ya hapo hakuna neno. Lakini bora kwa mwanamke ni yeye kujiepusha na kila kitu ambacho kinaweza kuwa ni fitina.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (13) http://binothaimeen.net/content/6776
  • Imechapishwa: 27/01/2021