´Awrah ya mwanamke si kama ´Awrah ya mwanaume. Bali ni khatari zaidi. Kutokana na hili tunasema kwamba ´Awrah ya mwanamke na mwanamke mwenzake ni kama ´Awrah ya mwanaume na mwanaume mwenzake. Lakini hiyo haina maana kwamba mwanamke avae mavazi yenye kusitiri baina ya magoti na kitovu tu. Hakuna mwanachuoni yeyote aliyesema hivi kabisa. Hata wanawake wa kizungu na wa makafiri hawafanyi hivi. Ni lazima wavae kitu kinachofunika  vifua vyao au angalau kwa uchache wanafunika matiti yao.

Hivi ni jambo linaloingia akilini Shari´ah hii ya Kiislamu iliyotakasika na inayotakasa inamruhusu mwanamke kutofunika isipokuwa yaliyo kati ya kitovu na magoti? Hili ni jambo haliingii hata akilini. Vazi la mwanamke linatakiwa kuwa lenye heshima.

Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) amesema kuwa mavazi ya wanawake wa Maswahabah manyumbani walikuwa wakivaa mavazi yaliyokuwa yakifunika kuanzia kwenye miguu mpaka kwenye mikono. Hapa ni pale wanapokuwa nyumbani. Ama wanapotoka Hadiyth mashuhuri inatambulika ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaruhusu kuyaburuza mavazi yao kiasi cha dhiraa moja ili wasitiri unyayo. Kwa hiyo vazi la mwanamke si sawa na vazi la mwanaume.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1056
  • Imechapishwa: 13/03/2019