Uwajibu wa muislamu kuijua dini kisha ndio abobee katika dunia

Swali: Je, unaonelea mtu abobee katika masomo ya kidunia badala ya masomo ya kidini pamoja na wakati huo huo mtu akashikamana na masomo ya kidini misikitini au muislamu abobee katika taaluma ya masomo ya kidini?

Jibu: Ni wajibu kwa kila muislamu ayajue mambo ya dini yake. Ni wajibu kwa kila muislamu ajifunze mambo ya dini yake anayoyahitajia. Ama kuhusu kubobea katika mambo ya kibiashara, ndoa na talaka, itategemea na kupenda kwa mtu. Lakini inatakiwa kuingia katika hayo baada ya kuijua vizuri dini yake. Baada ya hapo ndipo atachagua kile anachoonelea kuwa ni bingwa zaidi kama Fiqh, tiba, uhandisi, viwanda au kitu kingine chenye kuwanufaisha waislamu. Lakini jambo la kwanza mja anapaswa kuitambua dini yake. Anatakiwa kujua ni vipi atamuabudu Mola Wake, kuirekebisha ´Aqiydah yake, swalah, zakaah, swawm, hajj na namna ya kufanya ´Umrah. Pale atapoyajua vizuri mambo haya ndipo atachagua mwelekeo anaopenda. Allaah amewaumba watu na vitu mbali mbali wanavyopenda. Hili ni katika hekima ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Lau watu wote wangelikuwa na pendekezo moja basi kazi zingine zote zingeliharibika. Kila mmoja achague kile anachoona nafsi yake inapenda na azalishe kwacho. Ingawa ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote juu ya kwamba kubobea katika mambo ya dini ndio bora zaidi. Vilevile ni jambo zuri ikiwa atakabiliana masomo ya kidunia pamoja na kusoma kwa wanachuoni misikitini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-13.mp3
  • Imechapishwa: 12/06/2018