Uwajibu Wa Kumwambia “Yaahadiykumu Allaah” Anayepiga Chafya


Swali: Kumwambia “Yarhamka Allaah” anayepiga chafya ni wajibu na ni ipi dalili ya hilo?

Jibu: Kumwambia “Yarhamka Allaah” anayepiga chafya ni Sunnah. Ama kuhusu kumwambia “Yahadiykumu Allaah” ni wajibu. Akipiga chafya imependekezwa kumwambia “Yarhamka Allaah”. Ama kuhusu kumrudishia, bi maana kumwambia “Yahadiykumu Allaah” ni wajibu. Ni kama mfano wa kuanza Salaam ni Sunnah na kuitikia ndio wajibu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (42) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-03-10.MP3
  • Imechapishwa: 16/11/2014