Uwajibu wa kumwambia يهديكم الله anayechemua


Swali: Kumwambia:

يرحمك الله

“Allaah akurehemu.”

anayepiga chafya ni wajibu na ni ipi dalili ya hilo?

Jibu: Kumwambia:

يرحمك الله

“Allaah akurehemu.”

anayechemua ni Sunnah. Ama kuhusu kumwambia:

يهديكم الله

“Allaah akuongoze.”

ni wajibu. Akipiga chafya imependekezwa kumwambia:

يرحمك الله

“Allaah akurehemu.”

Ama kuhusu kumrudishia, bi maana kumwambia:

يهديكم الله

“Allaah akuongoze.”

ni wajibu. Ni kama mfano wa kuanza salamu ni Sunnah na kuitikia ndio wajibu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (42) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-03-10.MP3
  • Imechapishwa: 16/11/2014