Swali: Vijana wengi wametumbukia katika suala la kuwakufurisha watu kwa dhati zao pasi na elimu. Matokeo yake wakawakufurisha waislamu wengi. Vijana  hawa mara nyingi wanakuwa hawana elimu. Ni kipi kidhibiti cha hilo? Ni ipi hukumu ya kitendo cha vijana hawa?

Jibu: Hili ni kosa. Mwenye kupupia kukufurisha pasi na ujuzi wala elimu ni khatari sana:

“Mwenye kumwambia nduguye ´wewe ni kafiri` na asiwe hivo basi linamrudilia yeye neno hilo.”

Mwenye kusema ´ee kafiri`, ´ee fasiki`, ´ee adui wa Allaah` na mtu akawa hana sifa hiyo, basi neno hilo linamrudilia yule mtamkaji. Ni wajibu kwa mtu kuchunga ulimi wake. Asitamke isipokuwa kwa elimu na ujuzi. Takfiyr ina vidhibiti vyake kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Ni wajibu kwa mtu avijue.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/03.mp3
  • Imechapishwa: 29/09/2018