2- ´Ubaadah bin as-Swaamit (Radhiya Allaahu ´anhu) alisema kumwambia mwanawe:

“Ee mwanangu! Hakika hutopata ladha ya imani mpaka kwanza ujue kuwa yaliyokufika hayakuwa yakukukosa na yaliyokukosa hayakuwa yakukufika. Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Kitu cha kwanza alichoumba Allaah ni kalamu. Akaiambia: “Andika.” Ikasema: “Ee Mola Wangu! Niandike nini?” Akasema: “Andika makadirio ya kila kitu mpaka kitaposimama Qiyaamah.” Ee mwanangu! Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa salla) akisema: “Yule atakayekufa akiamini kinyume na hivi, basi huyo si katika mimi.”[1]

Mtoto wake anaitwa al-Waliyd bin ´Ubaadah bin as-Swaamit. Wakati ´Ubaadah alipokuwa anataka kukata roho ndipo mwanae akamuomba amuusie ambapo akamwambia amkaze na akasema:

“Ee mwanangu!”

Alisema hivo kwa sababu ya huruma na kumjali. Ni kama mfano wa Luqmaan aliposema:

يَا بُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ وَانْهَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Ee mwanangu! Simamisha swalah na amrisha mema na kataza ya maovu.”[2]

Baba anatakiwa kuwausia wanae juu ya kumcha Allaah (´Azza wa Jall) na kushikamana na dini na ´Aqiydah. Huu ni wajibu wa kina baba juu ya watoto zao. Ni lazima kwao kuwausia kumcha Allaah, kuzitengeneza ´Aqiydah na kushikamana barabara na dini na tabia nzuri.

[1] Abu Daawuud (4700). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (111).

[2] 31:17

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 596
  • Imechapishwa: 04/09/2019