Uuzaji wa chini ya kipaza sauti

Swali: Uuzaji wa chini ya kipaza sauti unaingia chini ya makatazo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Uuzaji juu ya uuzaji mwingine”?

Jibu: Hapana. Kilichokatazwa ni pale muuzaji atapotangaza kwamba yeye atazidisha na akataka kuuza mbele ya muuzaji mwengine kwa njia ya kwamba mteja anamwendea mtu mwengine na yeye anakuja na kumwambia asende kwake na kwamba yeye ana nyongeza. Haijuzu kwake kufanya hivo. Katika hali hii haifai kwako kusogea mbele na kumuharibia soko mwenzako ambaye mteja anataka kununua kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (66) http://alfawzan.af.org.sa/node/16524
  • Imechapishwa: 13/08/2017