Utumiaji wa kimakosa wa Jarh na Ta´diyl katika kuwaponda wanachuuoni wa Ahl-us-Sunnah


Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema “Mimi ni Salafiy”, bi maana yuko katika madhehebu ya Salaf, lakini anawaponda wanachuoni na kusema hii ni Jarh na Ta´diyl na amefanya hiyo ndio shughuli yake?

Jibu: Je, yeye ni mwanachuoni wa Hadiyth (Muhaddith)? Jarh na Ta´diyl ni elimu ya Hadiyth na elimu ya isnadi. Ama usengenyaji na uvumi ni haramu na sio Jarh na Ta´diyl. Ni kujeruhi ambako ni haramu na tunaomba kinga kwa Allaah. Ni usengenyaji na uvumi. Haijuzu kwake kufanya hivi. Je, Salaf walikuwa wanaruhusu usengenyaji na uvumi na kusema “Mimi ni Salaf”? Anasema uongo. Salaf hawakuwa wanaruhusu usengenyaji na uvumi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (67) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13854
  • Imechapishwa: 16/11/2014