Uteute kutoka kwenye tupu unachengua wudhuu´


Swali: Uteute mweupe unaomtoka mwanamke kipindi hana hedhi unachengua wudhuu´?

Jibu: Kila uteute unaotoka kupitia tupu ya mbele na tupu ya nyuma unachengua wudhuu´ kwa mwanamme na mwanamke. Amesema (Subhaanah):

وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ

”Mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu akitoka chooni au mmewagusa wanawake, kisha hamkupata maji, basi fanyeni Tayammum kwa ardhi ilio safi panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya mmoja wenu haikubaliwi anapopatwa na hadathi mpaka atawadhe.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Hadathi ni yale yote yanayotoka kupitia tupu ya mbele na tupu ya nyuma katika kinyesi, mkojo au uteute aina nyenginezo. Vivyo hivyo upepo unapotoka kwenye tupu ya nyuma. Lakini upepo unalazimisha mtu kutawadha tu: kuosha uso na mikono miwili, kupangusa kichwa na masikio mawili na kuosha miguu.

Ambaye ametokwa na kinyesi na uteute ni lazima kwake kujisafisha kwa maji kabla ya kutawadha juu ya vile viungo vinne vilivyotajwa. Hilo ni kutokana na udhahiri wa Qur-aan tukufu na Sunnah takasifu.

Mengine yenye hukumu moja kama upepo ni kula nyama ya ngamia, kulala na mengineyo yanayoondosha akili. Aidha kugusa tupu ya mkojo. Vichenguzi hivi vinalazimisha kutawadha peke yake na haikusuniwa kujisafisha kwa maji. Kuhusu kugusa tupu ni mamoja amegusa tupu yake mwenyewe au tupu ya mwengine kama mfano wa mke na mtoto.

[1] 05:06

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/131)
  • Imechapishwa: 21/08/2021