Uso wa maiti ndani ya kaburi lake unapasa kufunikwa

Swali: Je, kufunika uso wa maiti ndani ya kaburi lake ni jambo la lazima au imependekezwa?

Jibu: Unafunikwa uso wa maiti ndani ya kaburi na hauachwi wazi. Isipokuwa tu uso wa anayefanya Ihraam. Imepokelewa katika Hadiyth:

“Msimfunike kichwa wala uso wake. Kwani hakika Allaah atamfufua siku ya Qiyaamah hali ya kuwa ni mwenye kuleta Talbiyah.”

Amekataza kufunika kichwa cha Muhrim. Ama asiyekuwa Muhrim anatakiwa kufunikwa mwili wake mzima kukiwemo uso na kichwa chake. Vitafunguliwa vile vifungo kutoka kwa maiti na atabaki mahali pake kama alivyo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 15/08/2021