Masuala ya mwanamke kuonyesha mapambo yake, kuonyesha uso wake, nyimbo na ufisadi mbalimbali ulioko Saudi Arabia. Kadhalika masuala ya Bid´ah na benki za ribaa zilizoko Saudi Arabia. Muislamu anadhani kuwa ni vizuri na ni Sunnah yakawepo Ufaransa, Marekani, Yemen au kwengineko [lakini si Saudi Arabia]. Sivyo hivyo. Ichukue dini yako kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema, kama ilivyokuja katika “as-Swahiyh” ya Muslim:

“Hakika mimi nimekuachieni yale ambayo lau mtashikamana nayo barabara hamtopotea: Kitabu cha Allaah.”

Au Hadiyth yenye maana kama hiyo.

Chukua dini yako kutoka kwenye Qur-aan na Sunnah. Ama ufuataji kichwa mchunga unaofanywa hii leo unapelekea katika ufisadi. Huenda mtu wa kileo akadai kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah ilihali TV iko nyumbani kwake. Mtu wa kileo akadai kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah ilihali yuko na nyenzo ya kuchukua picha kando yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amewalaani wenye kutengeneza picha.”

“Kila mtengeneza picha ni Motoni.”

“Hakika Malaika hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa wala picha.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 334
  • Imechapishwa: 29/09/2019