Swali: Familia ya maiti wakifungua mlango wao kwa ajili ya wenye kuja kutoa pole pasi na kutendeka maovu yoyote – je, ni kitendo kinachojuzu?

Jibu: Hichi ni kitendo ambacho hakikupokelewa kwamba watu wakae nyumbani. Haikupokelewa kwamba watu wakae nyumbani na wakaacha makazi yao. Wanaweza kutoa pole popote walipo. Kwa mfano wanaweza kuwa dukani, kazini, njiani au msikitini. Hakuna haja ya kuweka sehemu maalum kwa ajili ya wenye kuja kutoa pole na sehemu hiyo ikatangazwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (15) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-24-11-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 07/09/2019