Usitangulie kujeruhi kabla ya wanachuoni


Utaona maneno kuhusu Ahl-ul-Ahwaa´ yameambatana na maneno kuhusu mapokezi. Baada ya kuandikwa Hadiyth kunabaki kuwazungumzia Ahl-ul-Ahwaa´, wa kale pamoja na wapya na wa sasa. Maimamu na wanachuoni (Rahimahumu Allaah) waliwashughulikia wale walioshi kabla yetu. Hawa ndio watambuzi wa kujeruhi. Wao ndio marejeo katika suala hili. Maneno yao ndio yanayotakiwa kurejelewa, na sio maneno ya wachanga, haijalishi kitu yale watayozungumza. Kwa hivyo ni wajibu kurudi kwa wanachuoni na kuwauliza ili waweze kuja na natija nzuri.

Jambo la kwanza wanatakiwa kujifunza adabu ili wasiwatangulie mbele wanahcuoni.

Jambo la pili ni usalama wa dini yao ili wasije kutumbukia katika jeuri. Huenda wakamzungumzia mtu kwa dhuluma. Huenda wakadhani kuwa maneno yao ni sahihi ilihali uhakika wa mambo sivyo hivyo. Iwapo wangeyarudisha maneno yao kwa mwanachuoni basi angeliwabainishia makosa yao katika hili.

Jambo la tatu ni manufaa. Pale anapozungumza mwanachuoni, watu wanayakubali. Ikiwa ni maneno yanayotoka kwa watu hawa, hakupatikani manufaa. Kwa ajili hiyo ni wajibu kwa watu wote kuyarudisha mambo haya kwa wale wastahiki na wamche Allaah.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=164632
  • Imechapishwa: 22/10/2017