Watu hawapendi kutamani yale wanayoyamiliki au yaliyomo kwenye mikono yao. Ukiingia kwenye nyumba ya mtu na ukaona kitu ulichokipenda na ikaonekana kuwa umependekezwa na kitu kadhaa na kadhaa, mtu huyo ndani ya nafsi yake atakuwa na kitu fulani. Jambo hili linapelekea kuharibu mapenzi.

Kwa hivyo, izoweze nafsi yako mambo ya watu kwako yawe ni duni yasiyokuwa na thamani yoyote kabisa. Haijalishi kitu ni vingi namna gani! Hili halipatikani isipokuwa kwa mtu mwenye moyo wa kuipa nyongo dunia ambaye ameufungamanisha moyo wake na Aakhirah na hajali mambo ya dunia.

Ama kuhusiana na mtu mwenye kuikodolea macho dunia, hutazama vilivyo kwenye mikono ya watu. Akitazama anavyomiliki huyu na yule, anavitamani. Hivyo huendelea kuomba na kuvikodolea macho na kuvitamani mpaka hatimaye watu wakawa hawampendi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 438
  • Imechapishwa: 12/05/2020