Swali: Matendo ya viungo ni sharti juu ya msingi wa imani au ni sharti juu ya kukamilika kwa imani?

Jibu: Inategemea. Kwa mfano kuacha swalah ni ukafiri. Kwa hiyo imani inalazimiana na kuswali. Hata hivyo mimi nawanasihi ndugu waache kupekua mambo haya na badala yake warejee katika yale waliyokuwemo Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Salaf walikuwa hawayatambui mambo haya. Muumini ni yule aliyefanywa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa muumini, na kafiri ni yule aliyefanywa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa kafiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-As-ilah al-Qatwariyyah, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 16/02/2019