Usiswali swalah ya ijumaa huko!


Swali: Kazini kwangu kuna umbali wa 140 km na nyumbani kwangu. Huko kuna msikitini ambapo naswali swalah ya ijumaa. Lakini Khatwiyb anawatukana Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Je, inajuzu kwangu kuacha kuswali swalah ya ijumaa katika msikiti huo? Kuna misikiti mingine, lakini hata hivyo iko mbali na kazini kwangu?

Jibu: Usiswali pamoja naye ilihali anawatukana Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hii ni dhambi kubwa. Usiswali pamoja naye. Swali Dhuhr. Usiswali swalah ya ijumaa. Isipokuwa ikiwa kama pembezoni mwako kuna misikiti mingine ambayo inaswali swalah ya ijumaa na hakuna makatazo mengine, swali kwenye misikiti hio.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (85) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17635
  • Imechapishwa: 28/06/2018