Swali: Ni upi muda wa juu zaidi mume kuwa mbali na mke wake akisafiri pamoja na kuzingatia kwamba amekuwa mbali kwa sababu ya kazi?

Jibu: Hapana shaka yoyote kwamba wakati mwingine mtu anaweza kulazimika kusafiri kwa ajili ya kutafuta riziki. Hata hivyo anatakiwa asiisahau familia yake katika likizo inayotolewa kwa ajili ya wafanya kazi. Kipindi hicho awatembelee kwa kadiri awezavyo. Asipotee mwaka au miaka miwili. Bali kukishapita mwaka achukue likizo inayotambulika na aitumie na familia yake. Hilo ndilo la wajibu kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/الفترة-القصوى-في-بعد-الرجل-عن-زوجته
  • Imechapishwa: 12/06/2022