Watu wamewaona Khawaarij kwa macho yao. Wameona namna wanavyoua na kufanya mauaji ya kinyama, wanaunguza na kuharibu, wanavunja na kuangamiza. Wakati yanapomalizika matendo ya Khawaarij utamuona huyu anamsalimia yule. Msimamo uko wapi? Mtu mwenye kuzusha katika dini ya Allaah haikustahikii wewe kupeana naye mikono. Haikustahikii wewe kumsalimia. Haikustahikii wewe kukaa naye. Kwa sababu amedhihirisha kile alichokuwa anaficha. Salaf walifanya hicho unachofanya? Hapana. Hicho mnachofanya kipo katika Qur-aan na Sunnah? Hapana. Vipi basi unaweza kuweka mkono wako kwenye mkono wake? Yako wapi mapenzi na chuki? Ikiwa watu hawa sio Khawaarij, Khawaarij wako wapi? Ikiwa watu hawa sio Khawaarij basi ulimwenguni hakuna Khawaarij. Wamefanya uasi kwa maneno na kwa silaha. Wana mfumo wanaoufuata. Wanaona kuwa wengine wote ni wapotevu. Ulimwenguni kuna mifumo mbali mbali lakini yote ni yenye kukataliwa na Allaah isipokuwa tu mfumo ambao umewekwa na Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ath-Thabaat ´alaa as-Swiraat al-Mustaqiym yakuun bil-´Ilm http://olamayemen.com/Dars-9998
  • Imechapishwa: 04/05/2018