Swali: Tuna Raafidhwah wengi kaskazini na khaswa kati ya waalimu. Waalimu tisa wa Raafidhwah wametujia huku Hafr-ul-Baatin. Unaweza kutoa fatwa dhidi yao au ukawatadharisha watu wa kawaida juu yao? Unapendekeza kutolewe Khutbah juu yao juu ya mimbari mbalimbali?

Jibu: Kuhusu fatwa dhidi yao, si yenye kutoka kwangu. Ni yenye kutoka katika baraza la kufutu. Wao ndio wenye jukumu la kufanya hivo.

Kuhusiana na kufunza, ni lazima kwa mtu aseme haki pasi na kujali iko kwa manufaa yake au dhidi yake. Ikiwa inadhihirika kwao kwamba wanalingania katika kitu kinachokwenda kinyume na madheheb uya Salaf, basi ni lazima wakatazwe kudhihirisha Bid´ah hii na wajadiliwe juu yake. Ni jambo linalotambulika kwamba wao na wengineo katika Ahl-ul-Bid´ah wakijadiliwa na wale ambao wana elimu juu ya Sunnah na madhehebu ya Salaf, watashindwa kukabiliana na haki. Kwani Allaah (Ta´ala) amesema:

بَلْ نَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَى الْبَاطِلِ فَيَدْمَغُهُ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ ۚ وَلَكُمُ الْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ

“Bali Tunaitupa haki juu ya batili inaitengua, tahamaki [batili hiyo inakuwa] ni yenye kutoweka na mtapata adhabu ya Moto kutokana na yale mnayoelezea.” (21:18)

Ama ikiwa mafunzo yao hayahusiani kitu na ´Aqiydah, kwa mfano iwe katika mambo ya hesabu, adabu au lugha na wala wasiingilie mambo ya ´Aqiydah, hakuna neno. Lakini ni lazima kwa mtu kuwa kujihadhari juu ya khatari ya Ahl-ul-Bid´ah ili Bid´ah zisitawanyike kati ya vijana wetu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (8 A)
  • Imechapishwa: 13/07/2021