Usimuoe mwanamke yeyote ila baada ya kujua dini na tabia yake


Swali: Je, nioe mwanamke ambaye sijui dini yake na kuwa ana ´Aqiydah sahihi au hapana? Kwa kuwa katika mji wangu kumeenea makaburi kuabudiwa.

Jibu: Usimuoe mwanamke isipokuwa baada ya kujua mambo yote kuhusu dini yake na tabia yake. Ulizia kuhusu yeye na soma hali yake. Usioe isipokuwa baada ya kuthibitisha kuhusu hali yake umjue kwanza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=126438
  • Imechapishwa: 22/09/2020