Usimuache mke wa kwanza kwa ajili ya kuongeza wa pili


Swali: Katika mji wetu haiwezekani kwa hali yoyote kuongeza mke isipokuwa kwa kukubali kwa yule mke wa kwanza ilihali na yeye hawezi kukubali. Je, mimi ni mwenye madhambi nikimpa Talaka na nikaoa mke mwingine pamoja na kujua kuwa ni mke mzuri?

Jibu: Haikutakikani kwako kuachana na mke huyu mzuri. Ni mke ambaye umewasiliana naye mwenyewe na ni mzuri, haikutakikana kwako kufanya hivi na kumuacha. Lakini ikiwa ni sahali kwako kuongeza juu yake mwingine, fanya hivyo. Ama kusema unaacha mke ambaye ni mzuri na kuenda kwa mwingine, na hali inakuwa namna hii baada ya huyu unaenda kwa huyu, hichi ni kitendo ambacho sio kizuri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarsubject&schid=9636&subjid=31339
  • Imechapishwa: 20/09/2020