Swali: Kuna mwanaume alimwamrisha mke wake kuporomosha mimba ambayo ilikuwa haijaeneza miezi mine ambapo mwanamke yule akamtii. Ni ipi hukumu ya kitendo hicho?

Jibu: Ikiwa kipomoko hakijapuliziwa roho, tutatazama. Ikiwa kunakhofiwa madhara juu ya mwanamke, basi hakuna neno akaiporomosha. Ama ikiwa hakukhofiwi juu yake madhara, si halali kwake kuiporomosha. Haijalishi kitu hata kama mume wake atamwamrisha. Kwa sababu yeye ndiye mwenye haki juu ya mtoto huyu. Lakini baadhi ya watu hawana hamu nyingine isipokuwa kukidhi matamanio yao tu. Huenda mtu huyu yuko na nia ya kumtaliki. Hivyo matokeo yake anachelea kuzaa ikawa ni kikwazo cha talaka. Kwa hivyo tunasema kwamba mwanamke haimlazimu kuporomosha mimba wakati mume wake atapomwamrisha kufanya hivo katika hali yoyote ile.

Ama ikiwa kipomoko hicho kimeshapuliziwa roho na kutimiza miezi mine, basi hii haifai kabisa kuiporomosha. Ni mamoja iwe kwa amri ya mume, daktari wala mwengine yeyote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (56) http://binothaimeen.net/content/1290
  • Imechapishwa: 13/10/2019