Swali: Kuna mtu ambaye baba yake kamuamrisha kumtaliki mke wake kwa sababu ya matatizo yaliotokea baina yake na familia yake mke. Ipi hukumu na je ni lazima kwangu kumtii baba katika hilo?

Jibu: Hapana. Sio lazima kumtii baba katika kumtaliki mke wake ikiwa anampenda. Isipokuwa tu ikiwa mke ana aibu ya Kishari´ah, hapo anaweza kumtaliki. Ama ikiwa ni mke mwenye msimamo na mzuri, lakini baba anamchukia kutokana na matatizo yalio baina yao au matamanio, asimtaliki mke wake kwa ajili ya kumtii baba yake. Hili ni jambo khususan kwa ´Umar. Pindi alipaomuamrisha Ibn ´Umar amtaliki mke wake na Ibn ´Umar akamuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akamuamrisha amtii baba yake. Hili ni jambo khususan kwa ´Umar. Ama wengine, hapana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/10070
  • Imechapishwa: 17/02/2018