Swali: Mwanamke anakataa kufanya jimaa na mume wake kwa hoja ya kwamba anamuabudu Allaah na kuwalea watoto. Je, inajuzu kwake kufanya hivo Kishari´ah?

Jibu: Hapana. Haijuzu kwake kufanya hivo. Bali mume wake anapomtaka ni wajibu kumuitikia. Isipokuwa ikiwa kama kuna kizuizi. Kama kwa mfano yuko na hedhi, damu ya uzazi, amefunga swawm ya faradhi kama nadhiri n.k. Inahusiana na swawm ya wajibu. Hata kama ni swawm ya Sunnah anatakiwa kuikata kwa sababu yake. Hatakiwi kumuasi mume wake kwa sababu hiyo:

“Mwanamke yeyote atakayeitwa na mume wake kitandani ambapo akakataa, basi Malaika wanamlaani mpaka kupambazuke.”

Malaika wanamlaani mpaka kuingie asubuhi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (71) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah26-07-1438h%20-%20Copy.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2017