Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ

“Hakika Sisi tumeiteremsha Qur-aan katika usiku wa Qadr.”[1]

Baadhi ya wanachuoni wamesema makusudio ya (القدر) ni utukufu na cheo. Wengine wakasema kuwa makusudio ya (القدر) ni makadirio kwa sababu katika usiku huo kunakadiriwa mambo yatayopitika katika mwaka. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ

”Hakika Sisi tumeiteremsha katika usiku uliobarikiwa – hakika Sisi daima ni Wenye kuonya –  ndani yake hupambanuliwa kila jambo la hekima.”[2]

Bi maana kunapambanuliwa na kubainishwa.

Sahihi ni kwamba neno hilo limejumuisha maana zote mbili. Hapana shaka yoyote kwamba ni usiku wenye utukufu na cheo kikubwa na pia ndani yake yanakadiriwa mambo yatayokuwa katika mwaka huo.

[1] 97:1

[2] 44:3-4

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr al-Qur-aan al-Kariym, Juz’ ´Amma, uk. 276
  • Imechapishwa: 14/05/2020