Usiku wa Qadr kwa mujibu wa Abu Bakrah

794- Humayd bin Mas´adah ametuhadithia: Yaziyd bin Zuray´ ametuhadithia: ´Uyaynah bin ´Abdir-Rahmaan ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia:

“Nilitaja usiku wa Qadr mbele ya Abu Bakrah ambapo akasema: “Mimi si mwenye kuutafuta wakati mwingine isipokuwa kutokana na vile nilivyosikia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika zile nyusiku kumi za mwisho. Hakika mimi nimemsikia akisema: “Utafuteni usiku wa tarehe tisa ni wenye kubaki, tarehe saba ni wenye kubaki, tarehe tano ni wenye kubaki au katika tarehe tatu ni wenye kubaki”[1]

Abu Bakrah alikuwa katika zile nyusiku ishirini za Ramadhaan anaswali kama nyusiku nyenginezo zote za mwaka. Kunapoingia zile nyusiku kumi za mwisho basi anajipinda.

Hadiyth hii ni nzuri na Swahiyh.

[1] Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (794).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Iysaa Muhammad bin ´Iysaa at-Tirmidhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jaami´ (793)
  • Imechapishwa: 15/05/2020