Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ

“Wanateremka humo Malaika na Roho kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo.”[1]

Wanashuka hatua kwa hatua. Kwa sababu Malaika ni wakazi wa mbinguni na mbingu ziko saba. Kwa hiyo Malaika wanashuka ardhini hatua kwa hatua mpaka ardhi inakuwa yenye kujaa. Kushuka kwa Malaika ardhini ni alama ya rehema, kheri na baraka. Kwa ajili hiyo mahali ambapo Malaika hawaingii ni yenye kukosa kheri na baraka. Kwa mfano zile sehemu ambazo zina picha.  Malaika hawaingii ndani ya nyumba ambayo ina picha. Zinazomaanishwa ni zile picha zilizoharamishwa, kwa sababu wanachuoni wengi wanaona kuwa picha ni zenye kufaa ikiwa picha hizo ni zenye kutwezwa kama kwenye mikeka au kwenye mito. Hivyo Malaika hawazuiliki kuingia sehemu hiyo:

وَالرُّوحُ

“… na Roho… “

Bi maana Jibriyl (´alayhis-Salaam). Allaah amemtaja yeye maalum ili kuonyesha utukufu na ubora wake.

[1] 97:04

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr al-Qur-aan al-Kariym, Juz’ ´Amma, uk. 275
  • Imechapishwa: 14/05/2020