Swali: Kuna mtu anachukulia wepesi swalah ya mkusanyiko pamoja na kuwa anatambua fika kuwa ni wajibu. Nimezungumza naye mara nyingi. Tatizo ni kuwa mimi naishi naye katika nyumba moja. Je, kuishi naye nazingatiwa kuwa nashirikiana naye katika dhambi hii?

Jibu: Huzingatiwi kuwa unashirikiana naye katika dhambi hii midhali unajitahidi Allaah kumwongoza kupitia mikono yako. Endelea kuishi naye na jaribu kumrekebisha na msaidie kumuamsha pale wewe unapoamka. Huenda Allaah akamwongoza kupitia mikono yako na hiyo ikawa ni kheri kwako na kwake.

Ama endapo ataendelea katika maasi hayo, mimi naonelea jitenge naye na utafute nyumba nyingine ili uweze kusalimika na shari yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (35) http://binothaimeen.net/content/778
  • Imechapishwa: 13/01/2018