Swali: Kuna mwanamke anataka kuhifadhi swawm ya jumatatu na alkhamisi na afunge siku kumi za Dhul-Hijjah. Lakini mume wake huenda akamkatalia juu ya hilo. Je, ana ruhusa ya kufanya hivo?

Jibu: Mwanamke hana ruhusa ya kufunga na mume wake hakusafiri isipokuwa kwa idhini yake. Haijalishi kitu jumatatu, alkhamisi, masiku meupe wala masiku kumi ya Dhul-Hijjah. Isipokuwa kwa idhini yake. Lakini haitakikani kwa mume kumzuia kutokamana na kheri na akabaki na kinyongo nafsini mwake. Akimruhusu kufunga amemsaidia katika kheri. Kusaidia katika kheri ni jambo zuri. Namshauri mume kumwacha akafunga. Lakini akiendelea kung´ang´ania na asimpe ruhusa itakuwa si halali kwa mwanamke kufunga ilihali mume wake yuko nyumbani isipokuwa kwa idhini yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (73) http://binothaimeen.net/content/1710
  • Imechapishwa: 18/04/2020