Usifungamanishe moyo wako kwa mwanamke

Swali: Ni ipi hukumu kwa ambaye moyo wake ameuambatanisha kwa dada mmoja wa Kiislamu na mwanamke huyo ni mmoja katika ndugu zake na anapangilia kumuoa huko mbeleni?

Jibu: Haitakiwi kwa mtu, khaswa inapokuja kwa mwanafunzi, akaumbatanisha moyo wake kwa mwanamke maalum na ikawa wakati wote akimfikiria yeye. Anachotakiwa ni yeye kumuomba Allaah amjaalie riziki yake aliyomuandikia juu ya kuoa iwe ya kheri. Anatakiwa kumuachia jambo lake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hili ni bora. Kitendo cha kuuachia moyo wako ukafungamana na mwanamke fulani ambapo ikamfikisha mtu katika mahaba, hili huenda hata likapelekea akapatwa na matatizo.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=jXHIORp8ejE
  • Imechapishwa: 19/09/2020