Swali: Kuna mtu alipanga miadi na mwenzake na yule mwenzake akawa amechelewa. Akampigia simu na kumuuliza sababu ya kuchelewa, akajibu ya kwamba nisiwe mwenye haraka, kwani Allaah ameumba mbingu [na ardhi] kwa siku sita na wewe unataka mambo yafanyike mnamo dakika tano. Je, maneno haya ni munasibu?

Jibu: Ndio, ni munasibu. Mambo yasichukuliwa kwa haraka. Mbingu na ardhi vimeumbwa mnamo siku sita pamoja na kuwa Allaah ni muweza wa kuviumba mara moja tu. Hapa kuna hekima ya Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (57) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-07.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020