Usidanganyike Na ´Ibaadah Nyingi Za Ahl-ul-Bid´ah – Kwani Zinatokamana Na Miongozo Ya Mashaytwaan!


Makusudio ya mwandishi – Imaam al-Aajurriy – ni kwamba usidanganyike na Ahl-ul-Bid´ah hata kama watapindukia katika kujipamba kwa Dini, kuipa nyongo dunia, kunyenyekea na kuswali. Usidanganyike nao kama ambavo usidanganyike vilevile na Khawaarij ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewasifu ya kwamba mtazidharau Swalah zenu mkizilinganisha na za kwao na visomo vyenu mkilinganisha na vya kwenu. Bi maana wamepetuka mipaka katika ´ibaadah.

Mtu wa Bid´ah akipetuka mipaka katika ´ibaadah basi tahadhari naye na usidanganyike kamwe na ´ibaadah zake. Bali kinyume chake zidi kujiweka naye mbali na kutahadhari naye zaidi. Hakika kujipamba kwake kwa Dini na ufanyaji wake wa ´ibaadah umejengwa juu ya kupetuka mipaka na fikira chafu na haukujengwa juu ya mfumo wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Khawaarij wamepetuka mipaka katika kuswali, kufunga, kusoma Qur-aan na kadhalika. Vilevile Maswahabah walikuwa wakizidharau Swalah zao wanapozilinganisha na za kwao. Lakini hata hivyo, je, hili liliwafanya wao kusifiwa? Liliwafanya kulaumiwa kwa sababu ni wapetukaji mipaka.

Kadhalika utaona Ahl-ul-Bid´ah wengi wana upetukaji mipaka katika kufanya ´ibaadah. Usidanganyike na upetukaji mipaka na kupindukia katika kufanya ´ibaadah kwa sababu tu wanaswali sana.

Jamaa´at-ut-Tabliygh wanaswali, wanamdhukuru sana Allaah, wanasafiri nchi na nyingine, lakini tazama Bid´ah na upotevu wao! Usidanganyike sawa ikiwa ni Jamaa´at-ut-Tabliygh, Tijaaniyyah, Marghaniyyah, Naqshabandiyyah, Sahrawardiyyah na mapote mengine katika Suufiyyah:

جُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً

“[Baadhi ya] Nyuso siku hiyo zitanyenyekea. Zenye kufanya kazi ngumu na kuchoka.Zitaingia na kuungua [kwenye] Moto mkali [uwakao] kabisa.” (88:02-04)

Ni wafanya ´ibaadah sana. Lakini pamoja na hivyo ni watu walio mbali kabisa na Dini ya Allaah. Kwa nini? Kwa kuwa wameenda kinyume na Mtume katika ´Aqiydah na Manhaj yake. ´Ibaadah zao ni zenye kurudishwa kwa kuwa hazitokamani na mwongozo wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). ´Ibaadah zao zinatokamana na miongozo ya Mashaytwaan wao na viongozi wao. Viongozi wa shari, Bid´ah na waovu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kwenda kinyume na Sunnah zangu sio katika mimi.” (al-Bukhaariy (5063))

Sunnah ni ukati na kati katika mambo yote. Miongoni mwa hayo ni ´ibaadah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/138-139)
  • Imechapishwa: 19/05/2015