Usichukue faida ya pesa zako ulizoweka benki


Swali: Yule ambaye anaweka pesa zake katika benki ya Ribaa na wala hachukui faida pesa zake zinazingatiwa kuwa ni za Ribaa au amesaidia tu katika dhambi na udui?

Jibu: Akihitajia kuhifadhi pesa zake katika benki ya Ribaa na wala asichukue faida hakuna neno. Kitendo hichi ni kwa minajili ya dharurah. Ama kuchukua faida za kiribaa haifai kwake. Kwa kuwa si yenye kumstahikia. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ

”Mkitubu basi mtapata rasilimali zenu – msidhulumu na wala msidhulumiwe.”[1]

Endapo atachukua ile faida na akaitoa swadaqah, basi si yenye kumstahikia. Anachotakiwa ni yeye kuchukua tu ile rasili mali yake. Akiichukua basi anachotakiwa ni yeye kuirudisha. Iwapo ataichukua basi anachotakiwa ni yeye kuitoa katika manufaa ya kijamii kwa nia ya kujinasua nayo na si kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah. Kuna watu ambao wanasema kuwa wanachukua ile faida na badala yake wanaitoa swadaqah. Hili ni kosa kwa njia mbili:

Ya kwanza: Wewe si mwenye kuiistahiki. Vipi utapewa nayo?

Ya pili: Shaytwaan ni mwenye kupupia wewe uichukue. Pale tu unapoichukua basi anakupendezeshea nayo na kukufanya wewe kutoitoa. Matokeo yake inakuwa mali yale.

Kwa hivyo ni wajibu kwa mtu kutochukua isipokuwa ile rasili mali yake. Mali yake ikiingiliwa na kitu katika Ribaa na asiweze kukirudisha basi anachotakiwa ni yeye kukitoa katika manufaa ya kijamii kwa nia ya kujikwamua nayo.

[1] 02:279

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 29/12/2017