Swali: Wapo baadhi ambao wameeleza kwamba imani maana yake ni kuzungumza kwa ulimi, kuamini kwa moyo na matendo ya nguzo na kwamba inapanda kwa kumtii Mwingi wa huruma na inashuka kwa kumtii shaytwaan. Je, maana hii imekamilika?

Jibu: Usibadilishe kitu. Leta maana ambayo wameafikiana kwayo waislamu. Usibadilishe matamshi. Imani ni kuzungumza kwa ulimi, kuamini moyoni na matendo ya viungo. Inapanda kwa utiifu na inashuka kwa maasi. Sema yale waliyosema.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (87) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-3-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2018