Swali: Ni ipi hukumu ya kutoa ushahidi wa uongo? Je, unabatilisha swawm?

Jibu: Kutoa ushahidi wa uongo ni dhambi kubwa. Nako ni kule mtu kutoa ushahidi kwa kitu asichokijua au kwa kitu anachojua kuwa kinaenda kinyume na uhalisia. Hakubatilishi swawm. Lakini hata hivyo kunapunguza ujira wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/360-361)
  • Imechapishwa: 13/06/2017