Swali: Je, kusengenya na kueneza uvumi kunamfunguza mfungaji mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Kusengenya na kueneza uvumi havifunguzi. Lakini hata hivyo vinapunguza swawm. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa kufunga kama ilivyofaradhishwa kwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule asiyeacha kusema uongo, kuutendea kazi na ujinga basi Allah hana haja yeye kuacha chakula na kinywaji chake.”

[1] 02:183

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/359)
  • Imechapishwa: 13/06/2017