Usende kwa msomaji Ruqyah asiyetambulika

Swali: Baadhi ya watu wanaweza kupatwa kwa wingi na maradhi ya viungo na ya kinafsi na matokeo yake wakaenda kwa wasomaji matabano. Wengi wao hawaponi. Ni zipi sababu za maradhi haya? Wapo ambao wanaamini kwamba yanatokana na majini au wakaamini kuwa ni uchawi. Ni zipi nasaha zako?

Jibu: Kwa hali yoyote maradhi yapo kwa watu, ni mengi na yako kwa aina mbalimbali. Ni wajibu kwa muislamu anapofikwa na maradhi aanze kusubiri, kutarajia malipo kutoka kwa Allaah na atambue kuwa haya yanatokana na mipango na makadirio ya Allaah. Asikate tamaa.

Pili haina maana kwamba asijitibishe kwa kufanya sababu kama na dawa zenye kusaidia. Haya ni mambo yanayofaaa akajitibisha kwa dawa zenye kufaa, matabano yanayokubalika Kishari´ah kwa watu wa Tawhiyd na watu wenye ´Aqiydah. Ama kwenda kwa wachawi, madajali na wale ambao lengo lao kubwa ni kula mali za watu na huku wanadai kuwa wanajua… yule asiyejulikana hali yake na kwamba ana ´Aqiydah sahihi na mfumo uliosalimika mtu asende kwake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayemwendea kuhani, mpiga ramli [katika upokezi mwingine ´mchawi`] na akamsadikisha kwa yale aliyoyasema, basi atakuwa ameyakufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammad  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Katika Hadiyth nyingine imekuja:

“Atakayemwendea kuhani basi hazitokubaliwa swalah zake kwa siku arubaini.”

Ameipokea Muslim.

Haijuzu kwenda kwa watu hawa madajali na waganga. Haijalishi kitu japokuwa watadai kuwa wanawasomea tu watu. Midhali hatuwajui, hatujui ´Aqiydah yao na hatuwaamini mia kwa mia, haifai kwenda kwao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (07) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/07.mp3
  • Imechapishwa: 04/01/2019