Usaliti na uhaini kwa manufaa ya Uislamu na waislamu

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anasaliti amana kwa manufaa ya Uislamu na waislamu?

Jibu: Huyu haitwi kuwa ni msaliti. Ambaye anafanya kwa manufaa ya Uislamu na waislamu haitwi kuwa ni msaliti wa amana. Anaitwa kuwa ni mtekeleza amana. Utekelezaji amana unakuwa kwa manufaa ya Uislamu na waislamu. Usaliti hauwi kwa manufaa ya Uislamu na waislamu. Uhaini wenyewe kama wenyewe ni shari. Lakini unafanywa kwa ajili ya manufaa ya Uislamu na waislamu sio uhaini. Ni kitendo gani hicho ambacho mwenye nacho amedhani kuwa ni uhaini?

Rushwa sio kwa ajili ya manufaa ya Uislamu na waislamu. Kuwaasi watawala sio kwa ajili ya manufaa ya Uislamu na waislamu. Kwa hiyo ni lazima kutazama jambo hilo. Ikiwa mtu ameamrishwa kumuasi Allaah basi asifanye hivo. Kwa sababu haijuzu kumtii katika maasi.

Ikiwa yale ya kwanza ndio makusudio yake basi atambue kuwa kitendo hicho hakiitwi uhaini. Huko ni kutekeleza amana. Asitii katika maasi na hivyo ndivo inavopelekea amana. Kwa msemo mwingine asimuasi Allaah. Amana juu yake ni yeye kumtii Allaah. Asipoitikia maasi basi ametekeleza amana. Haitwi kuwa amekhini amana.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4262/حكم-خيانة-الامانة-لصالح-الاسلام-والمسلمين
  • Imechapishwa: 14/06/2022