Usahihi wa maneno yanayosemwa mwishoni mwa mawaidha


Swali: Nawasikia baadhi ya walinganizi na watoa muhadhara wakisema mwishoni mwa mawaidha yao:

هذا ما عندي، فإن أحسنت فمن الله، وإن أسأت أو أخطأت فمن نفسي والشيطان

“Haya ni yenye kutoka kwangu. Kama nimefanya vizuri basi ni kutokana na Allaah, na kama nimefanya vibaya au kukosea ni kutokana na nafsi yangu mwenyewe na shaytwaan.”

Ni ipi hukumu ya kusema hivi?

Jibu: Sitambui ubaya wowote wa kufanya hivo. Huo ndio ukweli wa mambo. Mhadhiri, mwalimu, mhubiri na wengine katika watoa nasaha ni lazima kwao kumcha Allaah na kujaribu kuilenga haki. Wakipatia, basi hiyo ni fadhilah ya Allaah juu yao. Wakikosea, basi ni kutokana na upungufu wao na shaytwaan. Allaah na Mtume Wake wamesalimika kutokamana nayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/421)
  • Imechapishwa: 03/07/2021