Usaamah bin Laadin Na Wale Wenye Fikra Zake


Swali: Unajua kuwa Usaamah bin Laadin kahimiza vijana ulimwenguni nakusababisha ufisadi katika ardhi. Je, inajuzu kwetu kumsifu kuwa ni katika Khawaarij? Pamoja na kuzingatia kuwa anasababisha ulipuaji katika nchi yetu na nyinginezo.

Jibu: Kila ambaye ana fikra kama hii ni katika Khawaarij. Kila ambaye ana fikra kama hii na akalingania na kusisitiza watu kwayo ni katika Khawaarij, bila kujali jina lake na cheo chake. Huu ndio msingi. Ya kwamba kila yule ambaye analingania katika fikra hii, nayo ni kufanya Khuruuj kwa mtawala wa Waislamu, kuwakufurisha Waislamu na kuhalalisha damu ya Waislamu ni katika Khawaarij.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/33jOXMz_I5U
  • Imechapishwa: 09/11/2014